militantgoat (militantgoat) wrote in kiswahili,
haya, hapo chini kuna vitendawili. Vinanifurahisha sana na matumaini yangu ni kwamba mtavipenda pia! Kitu kingine cha kuwaambia, mimi mwenyewe sijua majibu! Pengine mtaweza kuvitafsiri na pia kutuambia mnafikiri majibu ni yupi.....

so here's a few riddles for you, just because they're fun and just because its Sunday evening. By the way, i don't know the answers! Perhaps people could post with their various translations of them and possible answers.....

vitendawili? tega!
vitendawili? tega!!


1. Nyumba yangu haina mlango

2. Nina watoto wangu ambao daima wanafukuzana lakini hawakamatani

3. Ninapompiga mwanangu hucheza

4. Nina saa ambayo haijapata kusimama tangu kutiwa ufunguo

5. Nzi hatui juu ya damu ya simba

6. Mzazi ana miguu bali mzaliwa hanayo

7. Nimewafugia wanangu milango wakati wanapopigana

8. Mti umeangukia huko mbali, bali matawi yake yamefika hadi hapa.

9. Po pote ninapoenda ananifuata

10. Daima yupo njiani anakwenda, bali bado hajafika mwisho wa safari yake.
  • Post a new comment

    Error

    Anonymous comments are disabled in this journal

    default userpic
  • 9 comments